Kanuni za Usalama na Afya Mahali pa Kazi za ILO
Kanuni za Usalama na Afya katika Sekta ya Ujenzi (Toleo Lililorekebishwa)
Toleo lililorekebishwa la Kanuni za Usalama na Afya za Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu usalama na afya katika sekta ya ujenzi lilipitishwa na Mkutano wa Wataalamu uliofanyika mjini Geneva tarehe 21 hadi 25 Februari 2022. Kanuni hizi zinachukua nafasi ya toleo la awali lililopitishwa mwaka 1992, ambalo lilionekana kuwa limepitwa na wakati kutokana na mabadiliko ya mbinu na hali za utendaji kazi katika sekta ya ujenzi katika miongo iliyopita. Toleo hili linazingatia maeneo mapya yanayohitaji maboresho ya hatua za usalama na afya mahali pa kazi pamoja na hatua nyingine za kujikinga.
Sekta ya ujenzi ni ya kimkakati kwa nchi wanachama wengi wa ILO, kutokana na uwezo wake wa kutoa fursa za ajira na uhusiano wake wa karibu na sekta nyingine za kiuchumi. Hata hivyo, sekta hii inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohusiana na hatari na vihatarishi vya usalama na afya mahali pa kazi.
Mwezi Februari 2022, mkutano wa wataalamu ulipitisha toleo lililorekebishwa la Kanuni za Usalama na Afya Mahali pa kazi za ILO kuhusu usalama na afya katika sekta ya ujenzi. Kulingana na viwango vya kazi vya kimataifa na taratibu za kisekta, kanuni hizi hutoa mwongozo wa namna ambavyo serikali, waajiri, wafanyakazi na wawakilishi wao wanapaswa kushirikiana ili kuondoa, kupunguza na kudhibiti vihatarishi na hatari kuu zote, kwa kuzingatia mabadiliko katika mbinu na hali za kazi katika sekta ya ujenzi.
Kanuni hizi zinasisitiza utekelezaji wa mifumo ya usimamizi wa usalama na afya mahali pa kazi (OSH) pamoja na ushirikiano kati ya waajiri na wafanyakazi pamoja na wawakilishi wao. Pia, zinakuza utamaduni wa kuzuia vihatarishi vya usalama na afya mahali pa kazi na kuhakikisha kunakuwa na mazingira salama na bora ya kazi katika hatua zote za mchakato wa mradi wa ujenzi.
Additional details
References
- ISBN Web PDF: 978-92-2