Mkakati wa Kukuza Kazi za Staha kwa Wafanyakazi wa Nyumbani
Mkakati wa Kukuza Kazi za Staha kwa Wafanyakazi wa Nyumbani (2025/2026-2029/2030) unaweka mwelekeo wa kutambua, kulinda na kuimarisha haki na mazingira ya kazi kwa Wafanyakazi wa Nyumbani nchini Tanzania. Unalenga kurasimisha ajira za nyumbani, kuimarisha ulinzi wa kisheria, kuimarisha wigo wa hifadhi ya jamii, kukuza ujuzi na kuhakikisha Wafanyakazi wa Nyumbani wanapata Kazi zenye Staha.